Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria

WATUMISHI WAPYA BODI YA MAJI BONDE LA ZIWA VICTORIA WANOLEWA MISINGI YA UTUMISHI WA UMMA

Imewekwa: 02 November, 2026
WATUMISHI WAPYA BODI YA MAJI BONDE LA ZIWA VICTORIA WANOLEWA MISINGI YA UTUMISHI WA UMMA

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria imetoa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa watumishi wapya walioajiriwa katika taasisi hiyo, kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu misingi ya Utumishi wa Umma, kuimarisha uadilifu na uwajibikaji, pamoja na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akifungua mafunzo hayo jijini Mwanza Oktoba 29, 2026, Meneja wa Huduma za Taasisi wa Bodi hiyo, Bw. Gideon Katalambula, amewataka watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, uadilifu, nidhamu na uwajibikaji, huku wakizingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazoongoza Utumishi wa Umma.

Amesema mafunzo hayo ni sehemu muhimu ya kuwaandaa watumishi wapya kuifahamu mifumo ya kiutumishi, wajibu wao na maadili ya kazi, ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Aidha, mafunzo hayo yanalenga kuwaimarisha watumishi katika kuwahudumia wananchi na wateja kwa weledi, uaminifu na kuzingatia viwango vinavyotakiwa katika Utumishi wa Umma.

Kupitia mafunzo hayo, Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria inaendelea kuimarisha uwezo wa watumishi wake na kujenga utumishi wenye weledi, uadilifu, nidhamu na uwajibikaji katika kuwahudumia wananchi.