Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria

Historia

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2000 kwa mujibu wa sheria Na. 42 ya Matumizi ya Maji ya mwaka 1974 pamoja na mabadiliko yake Na. 10 ya mwaka 1981. Hivi sasa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na 11 ya Mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake Na.8 ya Mwaka 2022.

 

Bonde la Ziwa Victoria linakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao millioni kumi na sita (16) hii ni kutokana na Sensa ya Taifa ya watu na makazi ya Mwaka 2022. Eneo zima la Bonde la Ziwa Victoria lina kilomita za mraba 115,400 na linajumuisha mikoa nane (8) ya Kagera, Mwanza, Mara, Geita, Simiyu na baadhi ya Wilaya katika Mikoa ya Shinyanga, Tabora na Arusha. Aidha vyanzo vya maji vilivyopo katika Bonde la Ziwa Victoria ni Ziwa Victoria, Rwakajunju, Burigi, Katwe, Rushwa na Ikimba, pamoja na mto Mara (Maji Shirikishi), Kagera (Maji Shirikishi), Grumeti (Maji Shirikishi), Mbarageti, Ngono, Simiyu, Isanga, Magogo Moame, Mirongo, Kanoni, Mori, Mabwawa na Maji chini ya ardhi.


Tunawakukaribisha kutembelea tovuti yetu na kushirikiana nasi katika jitihada za kulinda na kusimamia kwa uendelevu rasilimali za maji za Bonde la Ziwa Victoria.