Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria

BODI YA MAJI YA BONDE LA ZIWA VICTORIA YAENDELEA NA UTAFITI WA MAJI CHINI YA ARDHI ILEMELA.

Imewekwa: 02 November, 2026
BODI YA MAJI YA BONDE LA ZIWA VICTORIA YAENDELEA NA UTAFITI WA MAJI CHINI YA ARDHI ILEMELA.

Timu ya wataalamu kutoka Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Victoria inaendelea na shughuli za utafiti wa maji chini ya ardhi katika Mtaa wa Nyamadoke, Kata ya Nyamhongolo, Wilaya ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza.

Hadi sasa, jumla ya mitaa 15 imefanyiwa utafiti wa kitaalamu kwa kutumia mbinu za kisayansi za uchunguzi wa maji chini ya ardhi. Matokeo ya awali yanaonesha kuwa maeneo yote yaliyofanyiwa utafiti yana sifa zinazofaa kwa ajili ya kuendelea na hatua inayofuata ya uchimbaji wa visima virefu.

Zoezi hili ni sehemu ya juhudi za kuimarisha upatikanaji wa rasilimali za maji chini ya ardhi, kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi, pamoja na kuchangia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika Manispaa ya Ilemela.

Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Victoria inaendelea kutekeleza jukumu lake la kusimamia na kuendeleza rasilimali za maji kwa manufaa ya wananchi na maendeleo endelevu.