Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria

Tanzania yaahidi kuendelea kulinda Rasilimali za Maji

Imewekwa: 18 September, 2026
Tanzania yaahidi kuendelea kulinda Rasilimali za Maji

BOMET. Kenya:

Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja . Edward Flowin Gowele leo amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara Brigedia Jenerali  Evans Mtambi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mto Mara Nchini Kenya. 

Katika Hotuba yake aliyoisoma kwa niaba ya Mkuu huyo wa mkoa  ameeleza kuwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Serikali inaendelea kuimarisha usimamizi shirikishi wa Rasilimali za Maji ambao ndio msingi wa sera ya Maji,Ulinzi wa vyanzo vya maji pamoja na ufatiliaji wa mwenendo na ubora wa maji.

Mkuu huyo wa Wilaya ameeleza kuwa hatua hizo zinalenga kuhahakisha maji yanatumika kwa usawa, ufanisi na uendelevu huku ikizingatia mahitaji ya wananchi, shughuli za kiuchumi na mahitaji ya mazingira. 

Pia ametoa wito kwa serikali zote mbili , Taasisi , Jamii , sekta Binafsi na washirika wa maendeleo kuendelea kuimarisha ushirikiano katika kulinda na kusimamia rasilimali za maji katika Bonde la Mto Mara. 

Aidha ameitaka kamishen ya Bonde la Ziwa Victoria kuendelea kuratibu utekelezaji wa Hati ya Makubaliano iliyosainiwa mwaka 2012 kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kenya kuhusu usimamizi na uendelezaji wa Bonde la mto Mara, Pia kusimamia ukamilishaji wa Mpango wa pamoja wa matumizi ya Maji katika Bonde la Mto Mara (Joint Mara River Transboundary Water Allocation Plan)

Maadhimisho hayo yalifunguliwa tarehe 13 ya mwezi huu na kufika kilele leo katika viwanja vya Bomet vilivyopo kauti ya Bomet nchini Kenya. Huku viongozi mbalimbali kutoka ndani ya nchi ya Kenya na Tanzania wakishiriki.

Maadhimisho hayo hufanyika kila inapofika tarehe 15 ya  Mwezi Septemba ya kila mwaka