BODI YA TOA VIFAA KLABU ZA MAZINGIRA SHULE ZA MSINGI

Bodi ya maji ya Bonde la Ziwa Victoria imetoa vifaa vya usafi kwa klabu za mazingira katika shule sita za msingi katika wilaya za Muleba na Missenyi mkoani Kagera.

Zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo limefanyika katika shule za msingi za Bushekya,Bura, Ruhanga,Kyaka na Kassambya.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na keni za kumwagilia maji 30, mabuti 30, majembe 30, na miche ya miti ya matunda 1200.

Vifaa vingine ni pamoja na fulana, kofia, mipira na filimbi kwa lengo la kuhamasisha watoto kupenda kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kutunza vyanzo vya maji.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Afisa Maendeleo wilaya ya Missenyi ,Daudi Mlelwa alisema vifaa hivi vitaongeza hamasa kwa wanafunzi kutunza mazingira na vyanzo vya maji.

“Tunashukuru Bodi ya maji ya Bonde la Ziwa Victoria kutupatia vifaa hivi,hii ni kuonesha kwamba mapambano ya utunzaji wa mazingira na  vyanzo vya maji ndio imeanza.” Alisema Mlelwa.

Bodi ya maji ya Bonde la Ziwa Victoria imeshaunda klabu za mazingira katika shule za msingi sita na ambapo klabu hizo zinasimamiwa na walimu wa mazingira ambao wanawafundisha watoto umuhimu wa kutunza mazingira.

Klabu hizo zinajumla ya wanafunzi 180 ambapo kila shule ina wanafunzi 30 zoezi la uundaji wa klabu  katika shule za msingi linaendelea.

Updated: 17/08/2020 — 8:57 vm
Privacy Policy | Terms | Copyright © 2018 Lake Victoria Basin Water Board Website Developed By LVBWB