MKUTANO WA SEKTA NYINGI ZA BONDE

Mkutano wa sekta nyingi wa bonde.

Misingi ya mkutano
Mkutano wa sekta nyingi hufanyika kipindi ambacho Tanzania kama nchi imepata uzoefu wa Zaidi ya robo karne kuhusu jinsi ya kusimamia vyanzo vyake vya maji ikiongozwa na kanuni za IWRM.
Mipaka ya kihaidrolojia ikiwa kama vipimo vya makadirio, nchi nzima iligawanywa katika mabonde tisa ya mito na maziwa ikiwemo bodi ya maji bonde la ziwa Victoria iliyoanzishwa mnamo mwaka 2000 chini ya sheria ya matumizi ya maji (udhibiti na taratibu) nambari 42 ya mwaka 1974 iliyotenguliwa na nafasi yake kujazwa na sheria ya usimamizi wa rasilimali maji nambari 11 ya mwaka 2009.

Mkutano huu ni ari katika kuanzisha njia rasmi na yenye nguvu katika kuwahusisha washikadau mbalimbali katika wingi wao na pia kulisha taarifa kwenye bodi ya bonde la maji ambayo ni chombo kilichoundwa kisheria kilichopewa nguvu za kiutendaji katika usimamizi wa rasilimali maji katika bonde. Hii imetiwa chachu na sera ya maji ya mwaka 2002(NAWAPO) na sheria zinazoambatana nayo ambazo huainisha na kuongoza muelekeo wa sekta ya maji kwa siku za usoni na kufanikisha malengo ya usimamizi na maendeleo endelevu. Sera hii inatetea ugawaji wa majukumu ya usimamizi wa rasilimali maji kwa bodi za maji za mabonde(mito na maziwa), kamati za madakio na jamii za watuimia maji ukiwepo ushiriki hai wa washirika wa sekta mbalimbali.

Matumizi ya maji muktadha na hoja za kisekta.
Mara nyingi, sekta nyingi zinazohusisha taasisi nyingi hufanya kazi nyingi zinazotegemeana, zinazokinzana na zinazoingiliana katika mabonde ya mito na madakio. Makundi ya watumia maji maji mbalimbali katika madakio kama wamwagiliaji, wenye viwanda, wavuvi, wasambazaji maji, wafuaji wa umeme kwa kutumia maji, wamiliki wa maeneo ya burudani, misitu mazingira na jamii za mtaani, wote hawa hudai ya kuwa wanasimamia rasilimali maji lakini kwa jinsi inayowafaa kulingana na matumizi yao.
Matumizi mengi ya maji, watumiaji na wasimamizi wa maji wa aina nyingi ni viashiria kwamba usimamizi wa rasilimali za maji unahusisha wigo mpana wa maamuzi na watendaji ambao utendaji wao pasipo kuratibiwa vizuri ipasavyo inaweza kusababisha migogoro ambayo huleta madhara hasi kwa sekta husika, watumiaji wengine na huduma walizokusudia kuzitoa. Hii inashawishi kwamba maamuzi mazuri yanahitaji yafanywe kwa pamoja ili kuzidisha matokeo yanayohitajika, kupunguza matokeo yasiotakiwa na hivyo kupelekea matokeo endelevu ili kuondoa migogoro na kuendelea kutoa huduma zilizokusudiwa.
Hichi ndicho shughuli za IWRMD zinalenga kufanikisha na ndio sehemu kuu ya inayozingatiwa katika mikutano ya bonde na taifa ya sekta nyingi.

1.Malengo ya mkutano

1.1 Lengo kwa ujumla.
Lengo kubwa la mkutano ni kuwahusisha washikadau kutoka sekta mbalimbali kwenye kuongoza usimamizi wa rasilimali maji katika bonde.

1.2 Lengo maalum.
a) kuwajuza washikadau kuhusu mipango ya bonde na kuweka wigo wa kazi kwa washikadau wa hivi karibuni.

b) kufanya shauri na kuweka vipaumbele vya mipango na fursa zilizopo kwa ari za washikadau.
c)Kukubaliana kuhusu muudo na uongozi wa mkutano.

2. Matokeo yanayotarajiwa.
1. kuongezeka ufahamu wa washikadau kuhusu mipango ya bonde na ari ya uwakilishi wa wa washikadau waliopo kuhusiana na maji ikiwa ni msingi wa kuunganisha rasilimali na kusonga mbele.

2.Orodha ya kikundi kazi iliyokubaliwa kwa kipaumbele cha busara iliyoundwa kulingana na mipango ya bonde na ari za washikadau.

3.Muundo ulioridhiwa pamoja na uchaguzi wa viongozi ( pamoja na washiriki wa kikundi katika kazi).

3. Kazi na majukumu ya mkutano wa bonde.

3.1 Majukumu ya mkutano wa bonde.
Mkutano wa bonde unakusudia kujumuisha wadau wote wa rasilimali za maji. Mkutano huu unakuwa ni jukwaa la nidhamu anuwai ambalo litajadili na kufanya shauri kuhusiana na muunganiko wa simamizi za maji na maswala ya maendeleo yanayohusiana na matakwa mapana ya wadau, taasisi na sekta zinazohusiana na maji. Mkutano huu unatambulika kama njia ya kushauri jinsi ya kusimamia ongezeko la digrii za utata, utofauti na mienendo ya kimtizamo, hoja, umati wa mambo yaliyopuuzwa na unatumainiwa kuchochea ushirikiano na matokeo endelevu katika usimamizi wa rasilimali za maji. Kwa mtizamo wa mfanyakazi, mkutano huu umetambuliwa kama jukwaa la kusuluhisha matatizo kidemokrasia Zaidi katika usimamizi wa rasilimali za maji kwa kuondoa migogoro na kupelekea usimamizi wa maji kuwa wa ufanisi Zaidi.

3.2 Kazi za mkutano wa bonde.
Mkutano wa bonde unalo jukumu la kukamilisha shughuli zifuatazo, kati ya nyingine;

a) Kuishauri bodi ya bonde la maji kuhusu kupanga mipango, usimamizi, matumizi, kuendeleza, kulinda na kuhifadhi rasilimali za maji katika mabonde husika sambamba na majukumu na nafasi ya umma kuhusiana na shughuli hizo pamoja na athari zinazowezekana kutokea kwa jamii na mazingira.

b) kufanya shauri na kushiriki katika kupanga mipango na kuelezea maswala na changamoto zinazokabili usimamizi wa rasilimali za maji.

c) kusaidia katika kuratibu utekelezaji wa shughuli za watumia maji.

d)kusaidia uratibu na ushirikianaji wa jamii katika kutumia, kulinda, kuendeleza na kuhifadhi rasilimali za maji.

e) Mkutano utashauri kuhusiana na programu za sekta ya maji na maendeleo yanayohusiana na programu hizo ambayo huweza kuathiri au kuathiriwa na maendeleo ya sekta nyingine na hivyo kushauri jinsi ya kuoanisha maswala hayo.

f) Kushauri na kuhamasisha kulinda na kuhifadhi rasilimali za maji.

g) Kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi, mashirika yaliyojikita kijamii, mashirika ya jamii za kiraia,NGO’s, pamoja na makundi mengine yenye nia katika kulinda na kusimamia rasilimali za maji katika bonde.

h) Kushauri na kufanya utatuzi wa migogoro, makubaliano, mafunzo ya jamii pamoja na kufanya maamuzi jumuishi ili kupelekea usimamizi fanisi wa rasilimali za maji.

j) Kugawiana habari na taarifa, kubadilishana ujuzi, kujenga na kusambaza ujuzi kwa wadau.

Vikao, Taarifa(Ripoti) na Taratibu.
Mikutano ya bonde itafanyika katika misingi ya nusu mwaka na matokeo ya majadiliano yatapelekwa kwa BWO na kwenye mkutano wa Taifa (National Forum). Vikundi vya kazi vitakutana kila robo ya mwaka na kupeleka ripoti ya mikutano kwenye mkutano wa bonde kila nusu ya mwaka.
Baada ya kila kikao BWB husambaza muhtasari wa kikao kwa washiriki kwa ajili ya makubaliano na marekebisho kabla hazijasainiwa na mwenyekiti na katibu ndani ya siku saba za kikao. Mwenyekiti anao uwezo, kwa maombi ya washiriki(wanachama) au vyama vyenye nia mfano BWB wa kuitisha vikao maalum vya mkutano wa bonde au vikundi vya kazi katika muda wowote.

Programu ya mkutano.
Bonyeza linki hapo chini kuitazama programu ya mkutano

Updated: 07/10/2019 — 3:11 nm
Privacy Policy | Terms | Copyright © 2018 Lake Victoria Basin Water Board Website Developed By LVBWB