VIKUNDI KAZI

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria imefanya kikao kazi na vikundi kazi vya Jukwaa la Wadau wa Sekta Mtambuka jijini Mwanza.

Lengo la kikao kazi hicho kilichofanyika Januari 18, 2022 katika Ukumbi wa Ziwa Letu ilikuwa ni kuwakutanisha wadau hao ambao ni watumiaji wa maji ili kujadili na kuainisha fursa za rasilimali fedha zilizopo ambazo bodi inaweza kuzitumia katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji.

Akifungua kikao kazi hicho, Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Maji, Antony Dialo alisema njia hii ya kuhusisha watumia maji katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji ni sahihi na inayohakikisha upatikanaji wa suluhu ya pamoja.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Bodi,Dkt. Renatus Shinhu alisema bodi inavyanzo takriban 156 ambayo vimefanyiwa tathmini na kubaini changamoto mbalimbali zinazo vikabili vyanzo hivyo,ambapo mpaka sasa bodi imefanikiwa kuhifadhi vyanzo 12 tu na mpango kwa mwaka huu wa fedha ni kuhifadhi vyanzo vingine sita.

Alifafanua kuwa, kasi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na umuhimu wa rasilimali maji katika shughuli za kila siku za uzalishaji mali na mahitaji ya nyumbani, hivyo ushirikishwaji wa wadau katika kuchangia juhudi za uhifadhi ni jambo la muhimu.

Kikao kazi hicho kimeainisha fursa zilizopo kutoka kwa wadau mbalimbali ambazo bodi inaweza kuzitumia ili kuongeza mapato yatakayosaidia kuongeza kasi ya kuhifadhi na kulinda vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kuunda kamati ya kuhakikisha utekelezaji wa maadhimio ya kikao hicho.

Updated: 25/01/2022 — 10:43 am

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Privacy Policy | Terms | Copyright © 2018 Lake Victoria Basin Water Board Website Developed By LVBWB