Category: Uncategorized

THE LAUNCHING OF ZANZUI AND MWADILA WATER SOURCES CONSERVATION PROJECT IN MASWA DISTRICT

Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso Julai 29, 2022 amezindua miradi miwili ya uhifadhi wa vyanzo vya maji vya Zanzui (New Sola ) na Mwadila vilivyopo Wilaya ya Maswa. Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Aweso aliipongeza Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria kwa kazi kubwa waliyofanya ya kuhifadhi vyanzo hivyo kwa kishirikiana na viongozi wa Wilaya na jamii. “Usimamizi wa vyanzo vya maji ni shirikishi na hapa Zanzui na Mwadila mmeweza, inawapongeza sana,” alisema Waziri Aweso. Awali, akitoa taarifa ya miradi hiyo, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Bwana Renatus Shinhu alisema tayari Bodi imeweka mipaka ya kudumu katika chanzo cha Zanzui na wamesimika vigingi 250 kuzunguka eneo la chanzo hicho, pia kumepandwa miti 20,000. Mambo mengine […]

Privacy Policy | Terms | Copyright © 2018 Lake Victoria Basin Water Board Website Developed By LVBWB