Kategorie: Uncategorized

VIKUNDI KAZI

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria imefanya kikao kazi na vikundi kazi vya Jukwaa la Wadau wa Sekta Mtambuka jijini Mwanza. Lengo la kikao kazi hicho kilichofanyika Januari 18, 2022 katika Ukumbi wa Ziwa Letu ilikuwa ni kuwakutanisha wadau hao ambao ni watumiaji wa maji ili kujadili na kuainisha fursa za rasilimali fedha zilizopo ambazo bodi inaweza kuzitumia katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji. Akifungua kikao kazi hicho, Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Maji, Antony Dialo alisema njia hii ya kuhusisha watumia maji katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji ni sahihi na inayohakikisha upatikanaji wa suluhu ya pamoja. Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Bodi,Dkt. Renatus Shinhu alisema bodi inavyanzo takriban 156 ambayo vimefanyiwa tathmini na kubaini […]

MKUTANO WA SEKTA NYINGI ZA BONDE

Mkutano wa sekta nyingi wa bonde. Misingi ya mkutano Mkutano wa sekta nyingi hufanyika kipindi ambacho Tanzania kama nchi imepata uzoefu wa Zaidi ya robo karne kuhusu jinsi ya kusimamia vyanzo vyake vya maji ikiongozwa na kanuni za IWRM. Mipaka ya kihaidrolojia ikiwa kama vipimo vya makadirio, nchi nzima iligawanywa katika mabonde tisa ya mito na maziwa ikiwemo bodi ya maji bonde la ziwa Victoria iliyoanzishwa mnamo mwaka 2000 chini ya sheria ya matumizi ya maji (udhibiti na taratibu) nambari 42 ya mwaka 1974 iliyotenguliwa na nafasi yake kujazwa na sheria ya usimamizi wa rasilimali maji nambari 11 ya mwaka 2009. Mkutano huu ni ari katika kuanzisha njia rasmi na yenye nguvu katika kuwahusisha washikadau mbalimbali katika wingi wao na […]

Privacy Policy | Terms | Copyright © 2018 Lake Victoria Basin Water Board Website Developed By LVBWB