Karibu katika wavuti ya Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria. Sisi sote tunatambua umuhimu wa maji katika maisha ya kila siku ya binadamu na viumbe wengine. Maji ni Uhai, Maji ni Rasilimali muhimu sana katika kukuza na kuimalisha Uchumi wa Taifa katika uzalishaji mali. Tuunge mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muunagano wa Tanzania katika kuelekea Tanzania ya viwanda kwa kutunza na kuhifadhi Rasilimali hii.